Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:07

Amri ya kutotoka nje yatangazwa Maiduguri Nigeria


Gari lililochomwa moto katika kituo cha jeshi la anga mjini Maiduguri,Nigeria, Dec, 2. 2013.
Gari lililochomwa moto katika kituo cha jeshi la anga mjini Maiduguri,Nigeria, Dec, 2. 2013.
Serikali ya Nigeria imetangaza amri ya kutotoka nje kwa saa 24 katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri baada ya watuhumiwa wanamgambo wa kiislamu kushambulia kambi za kijeshi.

Jeshi la Nigeria linasema washambuliaji wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram walishambulia vituo vya jeshi na polisi nje kidogo ya mji wa Maiduguri mapema Jumatatu.

Lakini hapakuwa na idadi rasmi ya watu waliouawa au kujeruhiwa kutoka pande zote mbili. Hili ni shambulizi la kwanza kubwa katika mji mkuu wa jimbo la Borno tangu hali ya dharura kutangazwa mwezi Mei.

Uharibifu kutokana na shambulizi hilo ulionekana kilomita kadha kwenye barabara kati ya kituo cha jeshi la anga la Nigeria na makazi ya majeshi hayo. Umati wa watu wakiwemo watoto wadogo walionekana kuzunguka maiti iliyokuwa bado inateketea, na ambayo iliaminika kuwa ya mshambuliaji aliyekuwa kwenye basikeli.

Wakaazi wa eneo hilo walionyesha waandishi habari magari yaliyoteketezwa pamoja na taka zilizotapakaa barabarani wakisema ni mali ya washambuliaji. Pia waliwaonyesha maiti za wanaume wawili wakazi wa eneo hilo ambao walisema waliuawa kwa kupigwa risasi vichwani na washambuliaji.

Lakini majeshi na askari polisi walizuia waandishi habari kuingia kwenye vituo vyao kujionea kilichotokea baada ya mashambulizi hayo, ingawa moshi ulikuwa bado unaonekana kutokana na kile maafisa walisema ni magari yaliyochomwa moto.

Gavana wa jimbo la Borno Kashim Shettima ameahidi kujenga upya majengo yaliyoharibiwa katika shambulizi hilo na kusema kamwe serikali yake haitatetereshwa na vitisho vya washambuliaji hao.
XS
SM
MD
LG