Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:00

Amnesty inaripoti kuongezeka kwa ubakaji katika vitongoji Kenya


Shirika la haki za binadamu la Amnesty limetoa ripoti inayoeleza kwamba wanawake na wasichana wanaoishi katika maeneo maskini Nairobi wanakabiliwa na khofu ya kubakwa.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti kali mjini Nairobi, Kenya kuwa wanawake na wasichana wanaoishi katika mitaa duni ya watu maskini wanakabiliwa na khofu ya kubakwa na wakati mwingine kushindwa kutoka ndani ya nyumba zao wakati wa usiku kwenda kujisaidia.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Dr. Godfrey Odongo, wanawake wengi katika mitaa ya Kibira na Mathare mjini Nairobi wamegeuza nyumba zao na kuzifanya choo wakati wa usiku ili kuepuka adha ya kubakwa.

Kwa mujibu wa mfanyakazi wa shirika hilo la Amnesty International, Dr.Godfrey Odongo, amesema wengi wa wanawake wanaobakwa wanaishi katika hali duni ya maisha bila ya huduma muhimu za kibinadamu.

Serikali ya Kenya imelaumiwa vikali na shirika hili kwa kushindwa kushughulikia mahitaji muhimu ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na usalama wa kutosha. Eneo la Kibira linawakilishwa bungeni na Waziri Mkuu bwana Raila Odinga.

XS
SM
MD
LG