Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:22

Amnesty inaulaumu Umoja wa Mataifa kutowalinda wakimbizi Sudan


Wanajeshi wa Sudan.
Wanajeshi wa Sudan.

Amnesty inasema walinda amani walishindwa kuzuia majeshi ya Sudan kushambulia na kuwafukuza wakazi wa Abyei.

Kundi hilo la kutetea haki za binadam linasema walinda amani wa Umoja wa Mataifa walishindwa kuzuia majeshi ya Sudan kuwafukuza zaidi ya watu laki moja kutoka majumbani mwao katika mpaka wa kusini mwa nchi hiyo mwezi Mei iliyopita.

Amnesty International imesema wanajeshi wa Umoja wa Mataifa hawakuchukua hatua yeyote ya maana kuzuia majeshi ya Sudan na wanaharakati wanaowaunga mkono kushambulia nyumba za watu katika mji wa Abyei.

Katika ripoti Jumanne kuhusiana na matukio ya Mei iliyopita, kundi hilo lilisema, takriban wakazi wote wa Abyei walilazimika kukimbia makazi yao na kila kitu kilichokuwa na thamani mjini humo kiliporwa.

Kundi hilo lenye makazi yake London limesema, jeshi la Sudan liliripua daraja linalounganisha Abyei na Sudan Kusini ili kuwazuia watu kurudi katika makazi yao, na kueleza kwamba walinda amani wa Umoja wa Mataifa pia hawakufanya chechote kuzuia hatua hiyo.

Amnesty inasema baadhi ya walinda amani wa zamani wa Umoja wa Matiafa walikiambia kundi hicho kwamba uwamuzi ulichukuliwa kutopambana kijeshi na wanajeshi wa Sudan kwa sababu walikuwa na vifaa bora kuliko walonao wao.

XS
SM
MD
LG