Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Somalia wameanza shambulio la kijeshi dhidi ya eneo walilolieleza kuwa ni kambi kubwa ya mafunzo ya kijeshi ya wanamgambo wa Al-shabab nje ya mji mkuu wa Somalia.
Ofisi ya umoja wa Afrika huko Somalia AMISOM imesema katika taarifa yake jana kwamba operesheni hiyo ina lengo la kuteka kijiji cha Lanta Buro ,kilometa 40 magharibi mwa Mogadishu.
Maafisa hao wana matumaini kukiteka kijiji hicho kutasaidia kuleta usalama zaidi katika mji mkuu ambao unategemea kuwa mwenyeji wa mkutano wa baraza la katiba ambao una lengo la kumaliza miaka 12 ya utawala wa mpito huko Somalia.