Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:47

Al-Shabab washambulia wanajeshi Somalia


Al-Shabab Militants
Al-Shabab Militants

Wanamgambo wa kisomali kutoka kundi la al–Shabab Jumatatu wamevamia kwa ghafla wanajeshi wa serikali kusini mwa mji mku na kuwauwa zaidi ya darzeni. Al-Shabab kwa upande wao wamedai kuuwa zaidi ya wanajeshi 30 huku jeshi la Somalia likisema takriban wanajeshi 15 wa serikali ndio waliouwawa.

Wanamgambo hao pia wamesema kuwa waliteka malori kadhaa ya kijeshi wakati wa shambulizi hilo lilotokea kilomita 100 kusini mwa Mogadishu. Shambulizi hilo limetokea siku moja tu baada ya kundi hilo la wanamgambo kuua watu 12 kwenye hoteli mjini Mogadishu.

Wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wamekemea mashambulizi hayo wakiapa kuendelea kusaidia Somalia kupata amani na udhabiti. Wamesema kuwa mashambulizi hayo au hata mengine yatakayotekelezwa na wanagamgambo hayatashusha azma yao ya kusaidia Somalia.

XS
SM
MD
LG