Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:28

Al-Shabab latangaza mauaji kupitia Facebook


Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab

Wanaume hao watatu walipigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha cha Al-Shabab katika mji wa Barawe

Kundi la wanamgambo wa Somalia Al-Shabab limesema limeuwa watu watatu ambao linawashutumu kwa kufanya upelelezi katika mashirika ya kijasusi ya Marekani au Somalia. Kundi hilo lenye uhusiano na al- Qaida lilitangaza mauaji hayo Jumanne katika ukurasa wake wa Facebook.

Limesema mmoja wa wanaume waliouawa mwenye umri wa miaka 29 Mohamed Abdulle Gelle aliongoza ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kufanya shambulizi lililouwa kamanda wa Al- Shabab katika mji wa Juba nchini Somalia Oktoba mwaka jana.

Hilo likiashiria shambulizi lililomuuwa mtaalamu wa milipuko wa Al- Shabab aliyejulikana kama Anta, mwezi oktoba 28 mwaka jana.

Al-Shabab lilisema mtu wa pili, Ahmed Abudllahi Farole mwenye umri wa miaka 47 alifanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya jimbo la Puntland. Mwanamume wa tatu ambaye hakutambulishwa, alishtumiwa kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya Somalia.

Taarifa hiyo ilisema wanaume hao watatu walipigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha katika mji wa Barawe.
XS
SM
MD
LG