Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:03

al-Bashir hatosimamia tena uchaguzi wa rais Sudan .


Rais wa Sudan Omar al- Bashir katikati katika picha.
Rais wa Sudan Omar al- Bashir katikati katika picha.
Rais wa Sudan Omar al- Bashir amesema anapanga kujiuzulu mwaka 2015 baada ya miongo miwili kuwepo madarakani.

Katika mahojiano na gazeti la Qatari linaloitwa Al Sharq, lililochapishwa Jumatano , Bashir amerejelea uamuzi wake wa awali wa kutogombea katika uchaguzi ujao wa Sudan.

Alipoulizwa nini kitatokea kama chama chake kitamteuwa kama mgombea alisema hapana, miaka 20 ni mingi na kwamba watu wa Sudan wanataka kuona mtu mpya akiongoza.

Alisema chama tawala cha National Congress kitaamua kuhusu kiongozi mpya katika mkutano mwaka ujao.

Bwana Bashir mwenye umri wa miaka 69 ameongoza Sudan tangu mwaka 1989 alipochukua madaraka kwa njia ya mapinduzi.

Katika mahojiano yake hakugusia kuhusu mahakama ya kimataifa ya uhalifu ambayo imemshitaki kwa makosa ya uhalifu wa vita na mauaji ya halaiki dhidi ya raia katika mkoa wa Darfur nchini Sudan.

Bwana Bashir amepuuzia waranti ya kukamatwa ya ICC kwa kusafiri katika nchi marafiki kwenye bara la Afrika na Mashariki ya kati.
XS
SM
MD
LG