Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:27

Wanaharakati watetea haki za watu wenye HIV


Wanaharakati wa kutetea haki za kiraia kwenye mkutano wa 21 wa World Aids Conference, July 2016.
Wanaharakati wa kutetea haki za kiraia kwenye mkutano wa 21 wa World Aids Conference, July 2016.

Wanaharakati wa kisheria wanasema wana wasiwasi juu ya mwenendo unaoongezeka wa kuwaadhibu watu wenye HIV katika nchi nyingi ikiwa ni pamoja na Marekani.

Hakuna sheria inayojulikana ambayo si halali kwa mtu kuwa na HIV, lakini watetezi wa kutetea haki za binadam wanasema watu wenye virusi mara nyingi huonekana kama wahalifu.. Mataifa 72 yana sheria ambazo zinawahusu watu wenye HIV , nyingi zikuhusu utambulisho.

Kituo cha MArekani cha udhibiti na kuzuia magonjwa CDC, mwaka jana kiliripoti kuwa majimbo 24 ya Marekani yanawataka watu wanaofahamu kuwa wana HIV kueleza hali yao kwa wapenzi wao na majimbo 25 yanaadhibu hatua ambazo zina nafasi ndogo ya kuenenza virusi hivyo.

Maleche anasema, kwa hivyo sheria hizo zinamatatizo, kwa kuwa zinawanyanyapa watu ambao wanaishi na HIV, zinawapa watu wanaoishi na HIV mzigo mkubwa zaidi.

Hiyo ndio maana wakili wa kutetea haki za binadam mwenye makao yake mjini Nairobi Allan Maleche, ambaye alika katika meza moja na mawakili wengine katika mkutano na kutowa ushauri wa bure wa kisheria.

Maleche anasema anapigania ombi la rais wa Kenya la kuwepo orodha ya wazi ya watoto wote wanaoishi na HIV, jambo ambalo mawakili wanasema linakiuka sheria za kulinda ubinafsi. Anasema pia amewakilisha wagonjwa kadhaa wa kifuu kikuu walofungwa kwa kutokunywa dawa zao.

Bw. Maleche anasema, kesi yangu mbaya zaidi, ni kesi inayoendelea mbele ya Mahakama kuu ya Kenya, ni kuhusu madakatari wanaofunga uzazi wa wanawake wanaoishi na HIV bila ya ruhusa yao kwa sababu wanaamini wanawake wanaoishi na HIV ambao hupata mimba huwenda wakahatarisha maisha yao, kwa vile mfumo wa kinga ni dhaifu , na hivyo wanawafunga wanawake uzazi bila ya ruhusa. Huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadam mikononi mwa wafanyakazi wa huduma za afya ambao wanatakiwa kulinda haki za wanawake wanaoishi na HIV.

Katika mikutano kabla ya mkutano mkuu, shirika la kutetea haki za binadam AIDS Free World walitetea kesi ya nesi wa Uganda Rosemary Namubiru.

Namubiru alifungwa miaka 3 jela baada ya kudungwa kwa bahati mbaya na shindano na mama wa mtoto aliyekuwa akimtibu kunshitumu kwa kutumia tena shindano hiyo kwa mgojwa. Mtoto huyo wa kiume hakupatikana na HIV.

XS
SM
MD
LG