Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:46

Afrika yaendelea kudhibiti vyombo vya habari


Dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari, waandishi habari wa afrika wanaendelea kulalamika kutokana na kukandamizwa na serikali zao.

Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Dunia nzima inaadhimishwa kwa kutafakari na kuzungumzia manedeleo katika kuwapatia waandishi habari na vyombo vya habari uhuru ambao ni haki yao inayotambulika kimataifa.

Umoja wa Mataifa na mashirika yanayotetea haki za vyombo vya habari na waandishi habari yakiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari May 3, 2012, wanasema vugu vugu la upinzani katika nchi za Kiarabu ‘Arab Spring’, limepelekea serikali kupunguzwa udhibiti wao kwa waandishi habari, lakini wanasema pia mataifa mengi yangali yanakandamiza vyombo vya habari hasa huko Mashariki ya kati.

Katika sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York, katibu mkuu Ban ki-Moon amesema muongezeko wa sauti za vyanzo vipya vya habari katika nchi za Kiarabu kumechangia sana katika kuangushwa serikali za kimabavu.

Alisema mitandao ya kijami, simu za mikono na televisheni za seteliti zimewasaidia mamilioni ya watu kukomboa haki yao ya kwanza ya kidemokrasia. Lakini Bw Ban alilaani vikali mashambulio yanayosababisha mauwaji ya waandishi habari kote duniani akisema kuna zaidi ya waanidshi 60 walouliwa mwaka 2011.

Uhuru wa vyombo vya habari nchini Uganda ni swala ambalo linatiliwa maanani sana na katiba lakini waandishi wa habari wanalalamika kuwa uhuru huu umo kwenye vitabu tu. Hii ni kwa sababu kesi za kudhulumiwa kwa waandishi wa habari zinazidi kuongezeka kila mwaka.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kampala Leylah Ndinda, anaripoti kwamba shirika la wanaharakati wa kutetea haki za waandishi wa habari linasema vyombo vya usalama ndivyo vinavyowadhulumu sana waandishi wa habari.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Kutoka Dar Es Salaam, Hamza Kasongo mjumbe katika kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa muongozo na kanuni za wamiliki na vyombo vya habari, anasema tatizo kubwa Tanzania ni ukosefu wa madili ya kazi kutokana na kuenea kwa vyombo vingi vya habari

Kwa upande wao waandishi wa habari wa Kenya wamesheherekea siku ya kimataifa wakitafakari juu ya hatua za maendeleo walizofikia tangu nyakati za utawala wa chama kimoja cha siasa na kuongezeka kwa vyombo vya habari nchini humo.

Lempaa Suyianka mhariri katika shirika la utangazaji la KBC anasema moja kati ya matatizo makubwa kwa waandishi habari katika mashirika ya serikali ni kwamba hawa fanyi kazi katika mazingira inayostahki na baada ya mgomo wao mwzi Marchi kulalamika juu ya nyongeza za mishahara hakuna kitu kilichobadilika.

Kufuatana na ripoti iliyochapishwa Alhamisi na taasisi ya Freedom House yenye kutetea haki za vyombo vya habari, mjini Washington ni kwamba kati ya mataifa 197, ni mataifa 66 yaliyoorodheshwa kuwa na huru wa vyombo vya habari kwa mwaka 2011. Matifa 72 yalikua na sehemu ulani ya uhuru na mataifa 59 hayakuwa na uhuru wowote.

Kwa upande wa Afrika zaidi ya mataifa 13 yaliidhinisha sheria mpya za kudhibiti zaidi vyombo habari mwaka 2011, huku asili mia 10 pekee ndizo zilikua na uhuru kamili, asili mia 43 zilikua na sehemu ya uhuru na asili mia 43 bila ya uhuru wooet waq vyombo vya habari.


XS
SM
MD
LG