Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:09

Afrika Kusini yaitoa Afrika kimasomaso


Afrika Kusini ndiyo nchi pekee ambayo imelitoa bara la Afrika kimasomaso katika mashindano ya Olympic, Rio 2016 kwa sasa.

Mpaka sasa ni nchi pekee ya Afrika ambayo imeshinda medali mbili ambazo zote ni za fedha katika michezo ya kuogelea kutoka kwa Cameron Van Der Burgh na Chad le Clos.

Van Der Butgh alishinda medali yake katika kuogelea mita 100, wakati Chad le Clos alishinda katika mita 200.

Wachambuzi wanasema hali hiyo ya kukosekana kwa medali kwa Afrika mpaka sasa kunatokana na timu chache za Afrika kushiriki michezo iliyoanza katika Rio 2016.

Bara la Afrika linategemewa kufanya vizuri zaidi katika riadha, ndondi, na soka.

Timu ya kenya inategemewa kuiweka ramani ya Afrika katika riadha huku Nigeria ikitegemewa kufanya vizuri katika soka.

XS
SM
MD
LG