Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 23:46

Afrika Kusini: Wachimba madini haramu washambuliwa na wenyeji


Mtu anayeshukiwa kuwa mchimba madini haramu akipanda shimo la kutoa hewa ili kufika kwenye mgodi wa dhahabu ambao haufanyi kazi tena huko Benoni, mashariki mwa Johannesburg, Februari 17, 2014. Picha ya Reuters

Raia wa Afrika Kusini waliokasirishwa na uhalifu unaodaiwa kufanywa na wachimba madini haramu walifanya maandamano Jumatatu na kushambulia makazi kadhaa ya wafanyakazi hao, waandishi wa habari wa AFP wameshuhudia tukio hilo.

Zaidi ya watu 300 walikusanyika katika mji wa madini wa Mohlakeng, ulioko umbali wa kilomita 40 kutoka Johannesburg, waandishi hao wa AFP wameripoti.

50 kati yao wakiwa na mapanga na nyundo, waliingia katika nyumba tatu, na kuchukua magodoro, zulia, viti na kabati za nguo ambazo walizichoma moto.

Baadaye waliimba wimbo wa zamani wa wakati wa maandamano, ukimaanisha “ leta kikosi cha zima moto, kunawaka hapa,”, huku wengine wakinywa bia.

Magari kadhaa ya polisi yalifika sehemu hiyo nyakati za alasiri, na hali ya taharuki ilipungua baada ya mazungumzo kati ya waandamanaji na vyombo vya usalama.

Wachimba madini wasio rasmi, wanaoujikana huko Afrika Kusini kama “ zamas zamas”, wengi wao ni wageni wanaokuja Afrika Kusini kujaribu kupata pesa kwa kuchimba kwenye migodi isiyo rasmi, wakiishi na kufanya kazi katika mazingira magumu.

Hasira dhidi yao iliongezeka baada ya wanawake wanane kubakwa na wanaume wenye silaha tarehe 28 Julai, wakati wanawake hao walikuwa wanapiga picha ya video karibu na mji wa Krugersdorp, magharibu mwa Johannesburg.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG