Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:13

Afrika Kusini na Kenya waongoza kwa matumizi ya Twitter barani Afrika.


Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga akitoa hotuba mbele ya Rais wa Kenya na wabunge.
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga akitoa hotuba mbele ya Rais wa Kenya na wabunge.

Uchunguzi waonyesha Afrika kusini na Kenya ndio watumiaji wakuu wa mtandao wa Twitter barani Afrika.

Uchunguzi mpya unasema raia wa Afrika kusini na Kenya kuwa ni watumiaji wakubwa wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kwamba hivi sasa mtandao huo wa kijamii unakua haraka na kuwa nyenzo kubwa ya mawasiliano kwenye bara hilo.

Wachunguzi wametafiti zaidi ya twitt milioni 11.5 kutoka maeneo fulani ya Afrika katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2011.

Wamegundua Afrika kusini imetuma zaidi ya twitt milioni 5 , ikiwa ni mara mbili zaidi ya watu katika nchi nyingine. Kenya ilikuwa ya pili ikiwa na karibu milioni 2.5 , ikifuatiwa na Nigeria, Misri na Morocco.

Katika uchunguzi huo iligundulika asilimia 80 ya wale walioulizwa walitumia twitter kuwasiliana na marafiki zao, karibu asilimia 70 walitumia kupata habari na watu juu kidogo ya asilimia 20 walitumia mtandao huo kutafutia kazi.

XS
SM
MD
LG