Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:41

Afrika Kusini imeshtushwa na uwamuzi wa Uingereza kusitisha msaada


Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Justine Greening akiondoka afisi ya waziri mkuu huko No. 10 Downing Street London Sept. 4, 2012.
Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Justine Greening akiondoka afisi ya waziri mkuu huko No. 10 Downing Street London Sept. 4, 2012.
Tangazo la Uingereza lililotolewa siku ya Jumanne kwamba itasitisha misaada yake yote ya moja kwa moja kwa Afrika Kusini kuanzia 2015, limezusha malalamiko na mshangao mjini Pretoria.

Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Justine Greening alisema jana kwamba uingereza itasitisha msaada wa moja kwa moja kwa Afrika kusini unaokaribia dola milioni 29 kila mwaka. Greening amesema alishauriana na maafisa wa Afrika Kusini kabla ya uwamuzi kuchukuliwa na kwamba walikubaliana hivi sasa Afrika kusini imefikia kiwango cha kuweza kugharimia maendeleo yake wenyewe.

Hata hivyo mjini Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini maafisa wanasema walishtushwa na uwamuzi ulochukuliwa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Clayson Monyela alidokeza kwamba uwamuzi huwenda ukawa na athari kubwa katika uhusiano kati ya uingereza na Afrika Kusini.

"Serikali ya Afrika Kusini imepokea kwa masikitiko tangazo hili lililochukuliwa kipekee na serikali ya Uingereza kuhusiana na kusitisha kabisa msaada rasmi wa maendeleo kwa Afrika Ausini. Ni hatua muhimu yenye athari nyingi hasa kwa miradi ambayo inaendelea hivi sasa na inafikia hatua ya kutafakari upya ushirikiano wetu."

Monyela hakusema ushirikiano huo mpya utakuwa wa namna gani au utahusu nini. Nchi hizo mbili zinashirikiana katika masuala mbali mbali kupitia majukwa mbali mbali ikiwa ya kidiplomasia na mengineo.

Afrika kusini ni mshirika mkubwa kabisa wa biashara barani afrika. Na nchi zote mbili ni makazi ya idadi kubwa ya raia kutoka pande zote mbili.

Maafisa wa Afrika Kusini wanapenda kuringa, kwamba hadhi ya taifa lao limefikia kiwango cha taifa linaloinukia kiuchumi. Nchi hiyo imejiunga hivi karibuni na Jumuia ya mataifa yanayoinukia kiuchumi yanayojulikana kama BRICKS inayochanganya pamoja Brazil, Rashia, China na India.

Afrika Kusini pia ndio taifa kuu kiuchumi barani Afrika na nchi yenye idadi kubwa inayokuwa ya waafrika wa tabaka la kati.

Lakini licha ya mafanikio hayo yote msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Monyela, alieleza bayana kwamba Afrika ya Kusini haijaridhika na tangazo la ghafla la Uingereza.

Kuanzia sasa Monyela anasema serikali itabidi kutafakari juu ya namna ya kuendelea kugharimia baadhi ya miradi ya maendeleo vijijini iliyokuwa inasimamiwa na uingereza. Waziri wa Uingereza, Bi Greening anasema baada ya Uingereza kusitisha msaada wake 2015, mataifa hayo mawili yatazingatia juu ya biashara.
XS
SM
MD
LG