Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 02:02

Afrika Kusini: Chama kikuu cha upinzani chaanzisha hatua ya kisheria kuilazimisha serikali kumkamata Putin


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Russia Vladimir Putin wakihudhuria kikao cha kwanza cha mkutano kati ya Russia na nchi za Afrika katika mji wa mapumziko wa Sochi, nchini Russia, Oktoba 24, 2019.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Russia Vladimir Putin wakihudhuria kikao cha kwanza cha mkutano kati ya Russia na nchi za Afrika katika mji wa mapumziko wa Sochi, nchini Russia, Oktoba 24, 2019.

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini Jumanne kimechukua hatua ya kisheria kuilazimisha serikali kumkamata Vladimir Putin ikiwa Rais wa Russia atahudhuria mkutano uliopangwa kufanyika nchini humo.

Pretoria imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kidiplomasia tangu mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) ilipotoa hati ya kumkamata Putin, ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mkutano wa nchi wanachama wa BRICS mwezi Agosti.

Jumanne, chama cha Democratic Alliance kimesema kimeanzisha mchakato wa kuwasilisha ombi mahakamani kuhakikisha serikali inamkamata kiongozi huyo wa Russia na kumkabidhi kwa ICC ikiwa Rais Putin atafika nchini Afrika Kusini.

“Hatua hii ya awali ya kwenda mahakamani inalenga kuhakikisha kuwa Afrika Kusini inatekeleza wajibu wake,” Glynnis Breytenbach anayehusika na masuala ya sheria kwenye chama cha Democratic Alliance amesema katika taarifa.

Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa ICC, ina uhusiano wa karibu wa kidiplomasia na Moscow inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa BRICS ambao unajumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China, na Afrika Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG