Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:50

Wanasayansi waonyesha ramani ya maambukizo ya Ebola kutoka kwa wanyama


Ramani ya Afrika ikioonesha maeneo ambayo watu wana ambukizwa na virusi vya Ebola kutoka wanyama pori
Ramani ya Afrika ikioonesha maeneo ambayo watu wana ambukizwa na virusi vya Ebola kutoka wanyama pori

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford wameonyesha ramani ya maeneo ambako wanyama huenda wana maambukizo ya virusi vya ebola, ikiwa ni hatua ya kwanza kutabiri wapi ugonjwa huu utazuka hapo baadaye.

Wasanyansi wanasema kuzuka kwa ebola huko Afrika Magharibi kulianza wakati mtu mmoja alipokabiliana na mnyama aliyeambukizwa virusi hivyo. Pengine mnyama huyo huenda akawa ni popo. Wanaweza kuwa na virusi hivyo bila ya kuugua.

Dr. Nick Golding wa idara ya elimu ya wanyama katika chuo kikuu cha oxford anasema.

Dr. Golding anasema kuzuka kwa ebola kwa hakika kumewabainisha kwamba unaweza kuwa nitishio la afya ya umma. Ebola ina hatua mbili. Kimsingi, unaambukizwa kati ya wanyama huko msituni na unaweza kuambukiza binadamu wanapokuwa na mawasiliano na wanyama hao. Maambukizo ya aina hii ni kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Na halafu kuna usambazaji wa pili, ambao unaonekana huko Ghana na maeneo mengine ya afrika magharibi ambapo unaambukizwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu.

Anasema kusitisha mapema mlipuko wa ebola kwa binadamu ni muhimu kufahamu maambukizo ya awali kutoka kwa wanyama. Ramani iliyotolewa inaelezea takwimu ambako maambukizo ya binadamu na wanyama yametokea tangu mara ya kwanza kuzuka kwa ugonjwa huo mwaka 1976.

Dr. Golding anasema kwahiyo ramani waliyoitengeneza inaonyesha maeneo ambako wanadhani kuna hatari ya wanyama wenye maambukizo na hivyo ni hatari kwa binadamu.

Ramani inaonyesha kwamba idadi ya wanyama walioambukizwa huenda ikasambaa kote katika eneo kubwa la misitu huko Afrika ya Kati na Magharibi.

Anasema bahati mbaya hakuna takwimu za kutosha, kuhusu mahali walipo wanyama walioambukizwa au waliko binadamu ambao waliambukizwa siku za nyuma. Kwahiyo anasema walichofanya ni kuangalia mwenendo wa mazingira na kufananisha pale ambapo wamebaini kuwa mahusiano ya kimazingira – kwahiyo kwenye misitu kwa kutumia picha za satalaiti na viwango vya hali ya hewa na vigezo vingine. Anasema kimsingi wamefananisha sehemu kulingana na mazingira sawa na maeneo yale ambako virusi vya ebola vimegundulika kwa wanyama au binadamu wameambukizwa.

Mwasayansi wa Oxford anasema ramani hiyo inaonyesha maeneo makubwa ambayo awali yalidhaniwa kuwa na wanyama waliombukizwa ebola.

Kwa mfano, katika ramani za awali haikufikiriwa kuwa eneo hilo litakuwa afrika magharibi ambako mlipuko wa ebola umetokea hivi sasa. Maeneo ambayo yalikuwa katika hatari kubwa ni afrika ya kati – ambako ndiko mlipuko umetokea – huko jamhuri ya kidemokrasi ya congo.

Takriban watu milioni 22 wanaoishi katika nchi zilizoorodheshwa katika ramani, golding anasisitiza kwamba licha ya mlipuko wa karibuni, ebola bado ni maradhi yasiyo ya kawaida. Hata hivyo, baadhi ya maeneo yako katika hatari kubwa zaidi kuliko mengine. Na golding anasema kuelewa watu wapi wamekuwa na mawasiliano na wanyama wenye maambukizo ni muhimu sana katika kuzuia kuzuka kwa ugonjwa huu hapo baadae.

Kwahiyo Dr. Golding anasema ramani kwa hakika inaonyesha pale ambapo wanadhani huenda kuna wanyama walioambukizwa. Lakini hawana uhakika. Kwahiyo jambo bora ambalo linaweza kufanya ni kuanza kuwachunguza baadhi ya popo katika baadhi ya maeneo ambako ebola haijaripotiwa.

Anasema uchunguzi wa popo katika nchi ambako kesi za ebola hazijaripotiwa huenda ukaashiria hatari ya kuzuka kwa ugonjwa huo.

Katika maeneo hayo wanadhani kuna hatari, na katika nchi ambako maambukizo kwa binadamu yameripotiwa, na kuongeza uwelevu ni jambo muhimu sana katika mkakati wa kuzuia na kusitisha maambukizo ya mapema hapo baadae.

Virusi vya ebola vimegundulika kwa popo wa aina tatu, lakini wanasanysi hawajafuta uwezekano kuwa wanyama wengine huenda pia wakawa wananvyo virusi hivyo.

XS
SM
MD
LG