Utafiti mpya umebaini kwamba wananchi wengi wa Afrika wanapata fursa kubwa za uchumi lakini wanapoteza haki za kisiasa na usalama.
Ripoti ya kielelezo cha kila mwaka cha taasisi ya Mo Ibrahim juu ya utawala bora barani Afrika imetolewa Jumatatu. Watafiti wamegundua kwamba zaidi ya nchi 40 za Afrika zimepata mafanikio katika miaka mitano iliyopita katika maeneo mawili makuu, fursa za uchumi stahmilivu na afya na ustawi wa jamii.
Lakini watafiti wamesema mataifa 35 ya Afrika yalionesha kushuka kwa kiwango cha usalama na utawala wa kisheria. Nchi nyingine nyingi zimeshindwa katika eneo la ushiriki wa kisiasa na haki za binadamu.
Mwanzilishi wa utafiti huu mfanyabiashara wa Sudan, Mo Ibrahim alielezea matokeo kama mchanganyiko wa picha kuhusu mafanikio kuelekea utawala bora barani Afrika.
Utafiti ulitazama nchi za Mauritius, Ushelisheli, Botswana, Cape Verde na Afrika Kusini kama nchi zinazoendeshwa vizuri barani humo. Nchi tano za chini zilikuwa Eritrea, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Chad na Somalia.
Mo Ibrahim yaelezea utawala bora Afrika

Utafiti mpya umebaini kwamba wananchi wengi wa Afrika wanapata fursa kubwa za uchumi lakini wanapoteza haki za kisiasa na usalama.