Chombo cha habari cha serikali kimesema Jumapili, baada ya zaidi ya siku 100 ya kifo cha Mahsa Amini, kilichozusha machafuko.
Iran imekumbwa na maandamano ambayo serikali imeyataja ni ghasia toka kufa kwa Amini, 22 akiwa chini ya ulinzi hapo Septemba 16, baada ya kukamatwa kwa madai ya kukiuka kanuni kali za mavazi kwa wanawake.
“Afisa wa Basij aliuawa katika mji wa Semirom na wahalifu waliokuwa na silaha," shirika rasmi la habari la serekali IRNA liliripoti, likigusia kikosi cha kijeshi chenye uhusiano na idara ya walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu yenye nguvu.
Shirika la habari la IRNA limesema waandamanaji walikusanyika mwishoni mwa jumamosi katika mji huo, uliopo kilomita 470 kusini mwa mji mkuu Tehran.