Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:12

Afisa mwengine wa polisi afutwa kazi kwa kushiriki kumpiga kijana mweusi Memphis


Preston Hemphill afisa wa polisi aliye achishwa kazi.

Polisi wa mji wa Memphis katika jimbo la kusini mwa Marekani, Tennessee imewachukulia hatua za kinidhamu polisi sita kwa kushiriki kumpiga vibaya Tyre Nichols, na kumsababishia kifo kijana huyo mweusi baada ya kumsimamisha kwa kosa la barabarani.

Ofisa Preston Hemphill, amefutwa kazi katika jeshi la polisi, lakini bado hajafunguliwa mashtakata kwa makosa yoyote.

Polisi wa Memphis haikuweka wazi ushiriki wa afisa huyo wa polisi katika tukio la kumkamata na kumpiga Nichols.

Maafisa wengine watano wamefunguliwa mashatika kwa mauaji ya kiwango cha pili, kupiga, kuteka, kutowajibika na ukandamizaji wakiwa kazini.

Maafisa hao watano wote ni weusi na pia walifutwa kazi. Polisi ilitoa picha za video zikionyesha polisi watano wakimpiga vibaya Nichols mapema mwezi huu baada ya kumsimamisha barabarani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG