Takriban wakulima milioni 20 kwenye bara la Afrika watanufaika na mfuko huo wakati Afrika inakabiliwa na uhaba wa takriban tani milioni 30 za chakula, haswa ngano, mahindi na soya vinavyoagizwa kutoka Russia na Ukraine.
“Dola hizo bilioni 1.5 zitatumiwa kuzisaidia nchi za Afrika kuzalisha chakula na kufanya hivo kwa haraka,” rais wa AFDB Akinwumi Adesina ameviambia vyombo vya habari kabla ya mkutano mkuu wa kila mwaka katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
Mpango huo una lengo la kusaidia kuzalisha tani milioni 38 za chakula. Ni pamoja na tani milioni 11 za ngano, tani milioni 18 za mahindi, tani milioni 6 za mchele na tani milioni 2.5 za soya.
Mpango huo utatoa pia ufadhili na dhamana ya mikopo kwa ajili ya usambazaji mkubwa wa mbolea.