Adern ameyasema hayo kwenye ofisi ya makazi ya Maori kwenye mji wa Ratana nje ya mji mkuu wa Wellington, akiwa na mrithi wake na pia kiongozi wa chama tawala cha Labour Chris Hipkins.
Kiongozi huyo aliwashtua wakazi wa New Zealand pamoja na ulimwengu kwa ujumla baada ya kutangaza kujiuzulu wiki iliyopita, baada ya kuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 5, akisema kwamba hakuna alichobakisha kufanya.
Adern amekanusha madai kwamba alichukua hatua hiyo kutokana na chuki pamoja na na mashambulizi kupitia mitandao ya kijamii, kutoka kwa watu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, akiwaabia wana habari hakutaka mtu yeyote ayachukulie maamuzi yake kama ni ‘maoni mabaya kwa New Zealand.
Adern atabaki kuwa mbunge hata baada ya kuapishwa kwa Hipkins Jumatano, wakati chama chao cha Labaour kikikonekana kupoteza umaarufu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba.