Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:52

Adama Barrow aapa kufufua uchumi wa Gambia


Rais wa Gambia Adama Barrow baada ya kupata ushindi wa Decemba
Rais wa Gambia Adama Barrow baada ya kupata ushindi wa Decemba

Rais wa Gambia Adama Barrow, Jumatano ameapa kufanya kazi ili kufufua uchumi na kuhakikisha maendeleo yanaongezeka.

Hayo ameyasema baada ya kula kiapo cha kuanza muhula wake wa pili madarakani. Barrow mwenye umri wa miaka 56, aliingia madarakani mwaka 2017 baada ya kumshinda kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Yahya Jammeh.

Barrow kwenye uchaguzi wa mwezi uliopita lisinda kwa asilimia 53 ya kura zilizopigwa . Katika muhula wake wa kwanza, aliboresha mahusiano na mataifa mengi ya nje ambayo hayakuwa katika nafasi njema mzur wakati wa utawala wa Jammeh wa miaka 22. Barrow amejitahidi kurejesha uhuru wa watu ambao ulikuwa umekandamizwa katika kipindi chote cha nyuma wakatiw a utawala wa Jammeh

Alipoingia madarakani,alikabiliwa na changamoto ya kufufua uchumi wa taifa hilo dogo zaidi la barani Afrika. Janga la virusi vya corona liliusukuma uchumi kuingia katika msukosuko mwaka 2020 na kuwafanya watalii kutotembelea fukwe nzuri za taifa hilo.

XS
SM
MD
LG