Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:24

Rais wa Nigeria Umaru aombwa aachie ngazi


Mahakama moja ya Nigeria itasikiliza kesi tatu zinazodai rais anayeugua Umaru Yar’adua akabidhi madaraka kwa msaidizi wake.

Jaji Dan Abutu Jumanne alipanga tarehe 14 Januari kusikiliza kesi zote tatu.

Chama cha wanasheria wa Nigeria na mwanasheria mmoja maarufu Femi Falana na mbunge mmoja wa zamani wametaka makamu wa Rais Jonathan Goodluck ateuliwe kuwa rais wa muda.

Rais Yar’Adua yuko hospitali moja Saudi Arabia tangu Novemba 23 na hajaonekana hadharani wala kutoa maelezo yoyote kwa muda huo wote.

XS
SM
MD
LG