Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:37

Wakfu wa Mandela Wakanusha Madai


Wakfu wa mshindi wa tuzo la Nobel ya Nelson Mandela umekataa kuwa aliandika utangulizi kwenye kitabu cha kiongozi mwenzake wa Afrika.

Wakfu huo wa Mandela ulisema Jumanne kwamba rais huyo mstaafu hakuandika wala kusoma utangulizi wa kitabu hicho “Straight speaking for Africa.”

Kitabu hicho kiliandikwa na rais Dennis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Congo.

Utangulizi huo, unaodaiwa kuandikwa na bwana Mandela unasema bwana Sassou Nguesso ni kiongozi mashuhuri ambaye amejitahidi sana kuwakomboa waafrika wanaonyanyaswa.

Wakfu wa Mandela umesema maandishi hayo ni ‘dharau kubwa’ linaloshusha hadhi ya jina la bwana Mandela, na kwamba hatua inayostahiki itachukuliwa.

Mandela mwenye umri wa miaka 91 alifungwa jela kwa miaka 27 kwa kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Aliachiwa kutoka gerezani mwaka wa 1990 na hatimaye kuchaguliwa kama rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini mwaka wa 1994.

XS
SM
MD
LG