Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:56

Kibaki Afuta Uamuzi wa Raila


Rais Mwai Kibaki wa Kenya amefuta hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu Raila Odinga leo ya kuwasimamisha kazi mawaziri wawili, akisema hakukuwa na mashauriano yoyote katika swala hilo. Rais Kibaki alisema msingi wa kisheria aliotumia Waziri Mkuu haumpi madaraka ya kumfukuza au kumsimamisha waziri yeyote. "Kwa hiyo kikatiba, mawaziri hao wawili wangali madarakani." alisema Rais Kibaki katika taarifa kutoka Ikulu.

Saa chache kabla ya hapo Waziri Mkuu Odinga alitangaza mbele ya waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa amewasimamisha kazi kwa miezi mitatu Waziri wa Kilimo, William Ruto, na Waziri wa Elimu Prof. Sam Ongeri wakati uchunguzi unaendelea kuhusu shutuma za rushwa katika wizara zao.

Rais Kibaki alisema katika taarifa yake kuwa "hakukuwa na mashauriano yoyote" kati ya Rais na Waziri Mkuu katika swala la kuwasimamisha kazi mawaziri hao.

Kumekuwa na ripoti za maandamno katika mitaa ya mji wa Eldoret na miji mingine katika jimbo la Rift Valley baada ya Waziri Mkuu kuchukua hatua ya kuwasimamisha mawaziri hao. Wakati huo huo Mwanasheria mkuu nchini Kenya Amos Wacko amesema kuwa waziri mkuu hana haki ya kikatiba kuwasimamisha kazi mawaziri bila kushauriana na Rais wake. Mwanasheria mkuu huyo amesema Raila Odinga alikosea.

XS
SM
MD
LG