Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:23

Washington kutafakari na AU juu ya uchaguzi wa Sudan


Washington kutafakari na AU juu ya uchaguzi wa Sudan
Washington kutafakari na AU juu ya uchaguzi wa Sudan
<!-- IMAGE -->

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Afrika Michael Battle amesema serikali ya Washington itakua na majadiliano hivi karibuni na AU kutathmini uchaguzi mkuu wa Sudan ulokosolewa na wafuatiliaji wa uchaguzi wa kimataifa walodai haukufikia viwango vya kimataifa.

Balozi Battle anasema Marekani inasubiri kutoa uwamuzi wa mwisho juu ya uchaguzi huo hadi itakapomaliza kutafakari matokeo na AU. Wafuatiliaji wa uchaguzi wa Umoja huo walitangaza kwamba uchaguzi wa Sudan ulikua huru na wa haki.

Wafuatiliaji wa kimataifa ikiwa ni pamoja na taasisi ya Carter Center na Umoja wa Ulaya katika ripoti yao ya awali walieleza kua uchaguzi haukufikia viwango vya kimataifa. Marekani, Uingereza na Norway zilieleza katika taarifa kwamba uchaguzi uligubikwa na utayarishaji mbaya, kasoro zilizoonekana na kutoa wito wa kutekeleza kwa ukamilifu makubaliano jumla ya Amani ya 2005 (CPA).

Balozi Battle alisema wengi hawakutarajia upigaji kura utafanyika bila ya kasoro. Anasema hakuna aliyedhani utafanyika kwa vizuri kabisa. Huu ni uchaguzi wa kwanza baada ya robo karne anasema hivyo hapakua na matarajio ya kufanyika vizuri.

Tume ya uchaguzi ya Sudan ilitangaza matokeo ya mwisho yatachelewa kutolewa kutokana na kile tume imeeleza ni utaratibu wenye utata mkubwa. Hii imetangazwa baada ya matokeo ya awali kuonesha Rais Omar Hassan Al-Bashir anaongoza na anaonekana atabaki madarakani.


XS
SM
MD
LG