Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:57

Al Bashir aelekea kupata ushindi mkubwa


Al Bashir aelekea kupata ushindi mkubwa
Al Bashir aelekea kupata ushindi mkubwa

<!-- IMAGE -->

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Sudan yanaonyesha Rais Omar al-Bashir anaelekea kupata ushindi mkubwa. Ripoti kutoka mashirika ya habari ya Sudan zinaonyesha bwana Bashir anashinda kiasi cha asilimia 90 ya kura katika maeneo mengi na asilimia 97 huko kaskazini ya jimbo la Kassala.

Bwana Bashir alibashiriwa kushinda baada ya wapinzani wake wawili kutoka chama cha Umma na SPLM kujitoa katika kinyang’anyiro cha urais.

Vyama hivyo na vingine vinaishutumu serikali na chama cha NCP kwa kuiba kura.

Upigaji kura wa wiki iliyopita ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Sudan kwa kipindi cha miaka 24.

XS
SM
MD
LG