Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:50

Watu laki moja wahudhuria maziko ya Rais wa Poland


Watu laki moja wahudhuria maziko ya Rais wa Poland
Watu laki moja wahudhuria maziko ya Rais wa Poland

<!-- IMAGE -->

Siku ya mwisho ya shughuli za kumbukumbu ya Rais Lech Kaczynski na mkewe zilijumuisha ibada katika kanisa la St. Mary's Basilica katika mji wa kale wa kihistoria wa Krakow. Kanisa lilijaa familia na marafiki pamoja na maafisa wa serikali, viongozi wa kimataifa na wajumbe walohudhuria ibada hiyo.

Rais na mkewe walikuwa miongoni mwa watu 96 waliofariki wakati ndege waliokuwa wakisafiria ilipoanguka karibu na mji wa Smolensk, Rashia. Walikuwa wakielekea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuwakumbuka maafisa wa kijeshi elfu 22 wa kipolish waliouwawa na majeshi ya Russia mwaka 1940 kwenye msitu wa Katyn huko Russia Magharibi.

Katyn bado ni suala tete katika historia ya Poland na imetatiza sana uhusiano baina ya Russia na Poland.

Katika mazishi hayo spika wa bunge la Poland na ambaye pia ni kaimu rais, Bronislav Komorowski, alisema anatumai ajali hiyo ya ndege huwenda ikazileta nchi hizo pamoja.

"Kumekuwa na ishara nyingi njema na za maelewano kutoka kwa watu wa Russia na maneno na hatua za viongozi wa Russia. Haya yanashukuriwa sana".

Rais wa Russia Dmitri Medvedev alikuwa miongoni mwa viongozi wa kigeni walohudhuria mazishi hayo. Kabla kuondoka Krakow alisema yeye pia alitumai tukio hilo huwenda likaleta mabadiliko.

Viongozi wengi walipanga kuhudhuria mazishi hayo lakini walilazimishwa kuvunja mipango yao kutokana na ukosefu wa usafiri huko Ulaya hali iliosababishwa na wingu la jivu la volcano hewani kutoka Iceland. Rais Barack Obama alikuwa miongoni mwa wale ambao hawakuweza kuhudhuria.

Baada ya sherehe za mazishi majeneza ya Rais Kaczynski na mkewe yalipitishwa mjini kuelekea kanisa la Wawel ambapo walizikwa. Makundi ya watu walisimama barabarani huku wakirusha maua na kupeperusha bendera huku kengele ya kihistoria ya kanisa hilo ikiwaaga kwa mara ya mwisho.

XS
SM
MD
LG