Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:40

Vyombo vya habari Somalia vyahitaji msaada


Vyombo vya habari Somalia vyahitaji msaada
Vyombo vya habari Somalia vyahitaji msaada
<!-- IMAGE -->

kundi la kutetea haki za vyombo vya habari nchini Somalia limeeleza wasiwasi wake kwamba kuendelea kukosekana kwa usalama, kukaguliwa ripoti za vyombo vya habari na kukosa uungaji mkono wa kimataifa kwa waandishi wa habari nchini humo kunaweza kusababisha vyombo vya habari huru vya kujitegemea kutoweka kabisa .

Chama cha kitaifa cha waandishi wa habari nchini Somalia kimesema vyombo vya habari vya kujitegemea vilivyokua vikinawiri nchini humo vinaweza kutoweka ikiwa hali ya sasa ya kuvikandamiza itaendelea bila ya kuangaliwa.

Katibu mkuu wa kundi hilo la kutete haki za vyombo vya habari Omar Faruk Osman ameimbia Sauti ya Amerika-VOA, kwamba wajumbe wa makundi yenye nguvu ya kiislamu yenye msimamo mkali yanayoshirikiana na al-qaida ya al- Shabab na Hizbul Islam yametishia vyombo vya habari hivyo hadi kufikia kutekeleza amri zao na hivyo kuzusha wasiwasi kama watu wa Somalia wataweza tena kupata habari za uhakika.

Tangu mwaka 2007 wanamgambo wa kundi la al-qaida lenye ushirikiano na al- Shabab walichukua udhibiti kusini mwa Somalia na kuzuia vyombo vya habari katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao. Makundi hayo yanadhibiti vituo vya radio katika miji muhimu kama vile Baidoa, miji ya pwani na mji wa bandari wa kisimayo huko kusini.

<!-- IMAGE -->

Mapema mwaka 2009 kundi lingine lenye msimamo mkali la Hizbul Islam liliungana na al- Shabab katika juhudi zake za kutaka kuipindua serikali ya mpito huko Mogadishu. Licha ya uungwaji mkono na Umoja wa Mataifa na kuwepo kwa walinda amani 5,300 wa Umoja wa Afrika, serikali hiyo dhaifu imeshindwa kueneza udhibiti wake katika mji mkuu wa Mogadishu.

Osman amesema makundi yenye msimamo mkali yanataka kuweka sheria zao ngumu za kiislamu katika maeneo yote ya Somalia na wamelenga zaidi vyombo vya habari mjini Mogadishu kuwasaidia kufikia lengo lao. Amesema vyombo vya habari vya kujitegemea pia vinataabika kifedha kwa sababu wafanyabiashara wengi wanaogopa kununua nafasi za matangazo.

Somali ni moja ya eneo hatari duniani kwa waandishi wa habari kufanya kazi. Jumuiya ya waandishi wa habari wa somalia imesema takriban wafanyakazi 19 wa sekta ya habari wameuwawa tangu mwaka 2007.

XS
SM
MD
LG