Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:36

Wanawake wameshiriki kwa wingi uchaguzi Sudan


Wanawake wameshiriki kwa wingi uchaguzi Sudan

<!-- IMAGE -->

Licha ya matatizo na changamoto kadha zilizokumba uchaguzi wa Sudan, wanawake nchini humu inaelekea wana nia kubwa ya kutaka sauti yao isikike katika uchaguzi huu muhimu.

Ingawa itachukua siku kadhaa kujua idadi kamili, lakini matukio katika vituo vya upigaji kura katika siku tatu zilizopita yameonyesha kuna idadi kubwa ya wanawake wanaopiga kura kuliko wanaume. Ripoti kutoka maeneo mengine ya Sudan pia zinaonyesha kuwa wanawake zaidi wamepiga kura, wengi wao ikiwa ni mara ya kwanza katika maisha yao.

Naibu katibu mkuu wa chama tawala cha sudan kusini, SPLM, Ann Itto alieleza katika mkutano na waandishi wa habari jinsi alivyopiga kura.

"Ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yangu kupiga kura. Nilijisikia vizuri sana. Na nilihisi kuwa ninatoa mchango mkubwa katika kufanya taifa letu kuwa nchi zuri. Zaidi ya asilimia 70 ya watu katika msitari walikuwa wanawake, wengine waja wazito, na wengine wakiwa wamejifungua siku chache tu zilizopita".

Wanawake pia wameonyesha uvumilivu katika usumbufu wa kupiga kura. Katika sehemu nyingi wanaume walionekana kukasirishwa na kuondoka katika vituo vya kupigia kura wakati wanawake walifanya subira hadi kupiga kura zao.

Mpiga kura mmoja mwanamke ameiambia Sauti ya Amerika juu ya usumbufu aliopata katika kituo cha kupigia kura mjini Juba. Anasema baadhi ya majina katika vituo yaliandikwa kwa kiingereza na watu walishindwa kuyatambua majina yao kwa sababu hayakuandikwa kwa kiarabu.

Dr. Itto wa SPLM anasema wanawake, kama wanaume walipata usumbufu, lakini inaenelekea walikuwa na nia zaidi ya kupiga kura zao.

"Nia ya dhati niliyoiona katika nyuso za wasudan ambao walikuwa na nia ya kupata fursa ya kuchagua viongozi wao wa baadaye, ni nia ambayo SPLM inataka kuilinda".

Vilevile katika uchaguzi huu kuna idadi kubwa ya wanawake wanaogombania nafasi. Kulingana na kamati ya uchaguzi ya Sudan Kusini wanawake wapatao elfu moja wanawania nafasi katika uchaguzi huu. Na wanawake watatu wanagombania ugavana katika majimbo ya Equator ya Magharibi, Warrap na Unity.

XS
SM
MD
LG