Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:40

Ethiopia yawahukumu viongozi wa Oromo


Ethiopia yawahukumu viongozi wa Oromo
Ethiopia yawahukumu viongozi wa Oromo

Mahakama moja ya Ethiopia imetowa hukumu ya kifo kwa kiongozi wa kundi lililopigwa marufuku la Oromo linalopigania uhuru wao na kutoa vifungo vikali kwa watu wengine 15 kwa kupanga njama za kuipinduwa serikali.

Jopo la mahakimu watatu liliwapata washtakiwa 16 kwa kosa la kupanga njama dhidi ya serikali katika juhudi zao za kuanzisha taifa lao la Oromo. Waoromo ni kundi kubwa zaidi la kikabila nchini humo na lina asilimia 40 ya raia wa nchi hiyo.

Hukumu hizo zilitolewa wiki iliyopita lakini habari zilichelewa kutolewa kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya Pasaka.

Washtakiwa hao walikamatwa mwaka 2007 na 2008, na walishutumiwa kwa kuwa wanachama au wafuasi wa kundi la Oromo Liberation Front- OLF, ambalo serikali inalichukulia kuwa kundi la kigaidi.

Wengi wao walipewa vifungo vya miaka 10 hadi 13 bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Lakini kiongozi mshutumiwa wa kundi hilo Mesfin Abebe, alipewa hukumu ya kifo. Mshtakiwa mwengine Tesfahun Chemeda, alipewa kifungo cha maisha.

Miongoni mwa wale walioshutumiwa ni pamoja na wafanya biashara na wanasiasa mashuhuri. Wawili kati ya hao walikuwa ni wamiliki wa mahoteli makubwa huko Addis Ababa.

XS
SM
MD
LG