Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:59

Marekani inajaribu kuokoa uchaguzi Sudan


Marekani inajaribu kuokoa uchaguzi Sudan
Marekani inajaribu kuokoa uchaguzi Sudan

Maafisa katika wizara ya mambo ya nchi za njee hapa Washington wanasema bw Scott Gration amekwenda Sudan kwa ziara ya kujaribu kuokoa kile kinachotarajiwa kua uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi nchini humo tangu 1986. Gration aliondoka mapema wiki hii palipozuka tu, ishara za kua huwenda upinzani ukasusia uchaguzi wa rais unaotarajiwa kuanza April 11.

<!-- IMAGE -->

Tangu wakati huo chama tawala cha jimbo la kusini lenye madaraka ya ndani SPLM kimesema kitajiondoa kutoka uchaguzi kwa sababu za tuhuma za wizi wa kura uanopangwa na chama tawala cha National Congress, NCP cha rais Omar al-Bashir.

Vyama vingine vitatu vya upinzani vilitangaza jana kwamba vinajiondoa pia. Uchaguzi wa mwezi huu ni sehemu muhimu kabisa ya makubaliano jumla ya amani ya 2005, CPA, yenye lengo la kutanzua mzozo wa muda mrefu kati ya kaskazini na kusini.

Wakati wa mkutano na waandishi habari, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni P.J Crowley alisema kwamba, Gration baado anamini uchaguzi unaweza kuokolewa, akieleza hali ya kisiasa huko Khartoum kua ni ya kuyumba yumba akisema uwamuzi ulochukuliwa na makundi ya upinzani si ya mwisho.

“Lengo letu ni tayarisha uchaguzi wenye mashindano makubwa iwezekanavyo. Tunatambua hali ni ngumu sana. Haya ni masuala yenye utata mkubwa na magumu. Sudana haijapata kufanya jambo kama hili kwa muda mrefu. Lakini tunafahamu tatizo, liliyopo, na tunajaribu kulitanzua pamoja na vyama vyote. Tunataka kuhakikisha CPA inatekelezwa kwa ukamilifu”.

Crowley anasema uchaguzi wa rais ni hatua kubwa na muhimu kuelekea kura ya maoni wa mapema mwakani juu ya mustakbal wa kisiasa wa Sudan ya kusini na kuhakikisha inafanyika inavyostahiki itakua maendeleo makubwa kwa pande zote za kaskazini na kusini.

Afisa wa cheo cha juu wa wizara ya mambo ya kigeni aliyezungumza na waandishi habari alisema ususiaji hautakua kwa maslahi ya muda mrefu ya vyama vya upinzani vya Sudan ingawa anasema hadharau malalamiko yao kuhusiana na utaratibu wote.

Tasisi ya kimataifa inayohusika na mizozo ICG yenye makao yake Brussels ilikituhumu chama tawala cha National Congress kwa kujaribu kufanya wizi wa uchaguzi, ikisema NCP inapanga sheria za uchaguzi kujipendelea na kwamba takwimu zenye kasoro za idadi ya wakazi zimetumiwa kuchora mipaka ya wilaya.

Vyama vya haki za binadam navyo vinadai chama tawala kinawabughudhi na kuwashambulia wapinzani wake.

XS
SM
MD
LG