Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 19:51

Obama ahimiza kupitisha mswada wa mageuzi ya afya.


Rais wa Marekani Barack Obama anasukuma uungaji mkono katika hatua za mwisho katika kile alichokiita “mdahalo muhimu” hapa Marekani juu ya hatima ya huduma za afya wakati wabunge wakijiandaa kwa kura hiyo muhimu.

Bw. Obama aliuambia mkutano wa hadhara nje kidogo ya Washington kuwa kama kura katika baraza la wawakilishi ikishindwa kupatikana Jumapili sekta ya bima itaendelea kuwa haidhibitiki na gharama za huduma za afya zitaongezeka hapa Marekani.

Amesema kura ya ndio katika mageuzi ya huduma za Afya itakuwa ushindi kwa wananchi wa Marekani.

Wabunge wa baraza la wawakilishi wanatazamiwa kupiga kura muhimu siku ya Jumapili kuidhinisha mswada ulojadilikwa kwa takriban mwaka mzima juu ya namna ya kupunguza gharama za huduma za afya na kuhakikisha wamarekani wote wanaweza kupata bima ya afya kwa beiu nafu.

XS
SM
MD
LG