Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 21:07

AU ina wawekea vikwazo viongozi wa Madagascar


Braza la amani na usalama la Umoja wa Afrika lilikutana Jumatrano na kutangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa Madagascar wanaokaidi wito wa Jumuia ya Kimataifa kutanzua mzozo wa kisiasa wa kisiwa kikuu cha bara la afrika Madagascar.

Kamishna wa amani na usalama wa AU Ramtane Lamamra alisema Umoja wa Afrika umemuekea Rais Andry Rajoelina pamoja na washirika wake wakisiasa 108 vikwazo vya kutosafiri nje ya nchi na kuzuia mali zao katika mabenki ya kigeni na kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuwatenga maafisa hao upande wa kidiplomasia.

AU ilikua imempatia rais wa Madagascar mwezi mmoja tangu Febuari 16 kutekeleza makubaliano ya kugawanya madaraka yaliyofikiwa na upinzani mwaka jana au kukabiliwa na vikwazo. Rais Rajoelina alipuuzi onyo la Umoja wa Afrika na kukata mwaliko wa AU kuhudhuria mkutano wa upatanishi mapema mwezi huu.

Wapatanishi wa kimataifa wamekua wakihimiza kuundwa kwa serekali ya umoja wa kitaifa na uchaguzi mpya tangu Bw Rajoelina kunyakua madaraka kutoka kwa rais Marc Ravalomanana mwaka mmoja uliyopita.

XS
SM
MD
LG