Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:55

Mabadiliko ya serikali DRC haijawaridhisha waasi


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amefanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri mwishoni mwa wiki kwa kupunguza idadi ya wajumbe wake. Baraza hilo lina mawaziri 44 badala ya 54 walokuwepo, na waziri mkuu anabaki katika wadhifa wake.

Uwamuzi huo unapongezwa na baadhi ya wachambuzi wa kisiasa kua ni hatua nzuri ya kupunguza matumizi ya serekali kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Lakini makundi kadhaa ya waasi huko mashariki ya Kongo yanadai mabadiliko yanakwenda kinyume na makubaliano ya amani ya Goma.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Didier Bitaki kiongozi wa kundi la Mai-Mai kifuafua, anasema kundi lao halijaridhishwa kwa sababu walikubaliana huko Goma mwezi Machi mwaka jana walipotia saini mkataba wa amani kwamba, baada ya wapiganaji wa makundi mbali mbali kuingizwa katika jeshi la taifa, utaratibu wa kuwahusisha viongozi wao katika siasa na serekali utanaza.

Bw Bitaki aliongeza kusema kwamba, walipokutana mara kadhaa na mafisa wa vyeo vya juu hasa rais na mawaziri wake, hawakukata kamwe juu ya kuwahusisha katika serekali.

Hata hivyo vyombo vya habari vya kongo vina wanukulu maafisa katika afisi ya waziri mkuu wakisema kwamba, hapatakua na nafasi za mawaziri kwa makundi ya zamani ya waasi ambayo wapiganaji wao wameingizwa katika jeshi la taifa.

Lakini Bitaki anasema serekali imeshindwa kushughulikia matakwa ya kundi lake. Wapiganaji hao wa zamani wanaomba nafasi nne katika baraza la mawaziri.

Hata hivyo kwa upande wake waziri wa habari Lambert Mende anasema waasi wazamani wanabidi kuzingatia kwanza katika kuunda vyama halali vya kisiasa kuweza kushiriki katika uchaguzi wa mwakani kama vyama vingine.

Anasema hunyakuwi wizara hivi hivi. Ni lazima uwe mwanachama wa chama cha kisiasa ambacho kina katiba yake na kimesajiliwa, na kufuata utaratibu wa sheria.

Bataki anasema waasi watarudi msituni kupambana na serekali ya Kinshasa ili kuweza kutanzua matatizo yao.

XS
SM
MD
LG