Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:41

Ratiba ya Kombe la Afrika 2012 Yapangwa


Nchi za Afrika Mashariki na Kati zimepangwa katika makundi magumu ya michuano ya awali ya kombe la mataifa Afrika 2012, kulingana na ratiba iliyotangazwa Jumamosi Lubumbashi.

Timu ya taifa ya DRC imepangwa katika kundi gumu la 5 ambalo tayari linaitwa "kundi la kifo" pamoja na timu za Cameroon, Senegal na Mauritius. Tanzania iko katika kundi la 4 pamoja na Algeria, Morocco, na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kenya na Uganda ziko katika kundi moja la 10 pamoja na timu za Angola na Guinea Bissau. Burundi na Rwanda pia zimewekwa kundi moja la 8 kuchuana na timu za Ivory Coast na Benin.

Mabingwa watetezi Misri wamewekwa kundi moja na Afrika Kusini pamoja na Sierra Leone na Niger katika kundi la 7 ambalo linatazamiwa kuwa moja ya makundi magumi. Michuano ya awali inaanza Septemba mwaka huu wakati fainali itafanyika Januari 2012 huko Gabon and Equatorial Guinea.

Kuna makundi 11 katika michuano hiyo ya awali. Washindi wa kila kundi na timu tatu zitakazochukua nafasi za pili kwa rekodi nzuri zitacheza katika fainali ya Januari 2012.

Makundi kamili:

Kundi 1: Mali, Cape Verde, Zimbabwe, Liberia.

Kundi 2: Nigeria, Guinea, Ethiopia, Madagascar

Kundi 3: Zambia, Mozambique, Libya. Comoro

Kundi 4: Tanzania, Algeria, Morocco, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kundi 5: DRC, Cameroon, Senegal, Mauritius

Kundi 6: Burkina Faso, Gambia, Namibia, Mauritania

Kundi 7: Misri, Afrika Kusini, Sierra Leone, Niger

Kundi 8: Rwanda, Burundi, Ivory Coast, Benin

Kundi 9: Ghana, Congo, Sudan, Swaziland

Kundi 10: Uganda, Kenya, Angola, Guinea Bissau

Kundi 11: Tunisia, Malawi, Chad. Botswana

XS
SM
MD
LG