Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 03:49

Mapinduzi ya kijeshi Niger


Akilihutubia taifa kupitia vyombo vya habari, msemaji wa wanajeshi waloasi amesema wamesitisha katiba ya nchi na kuivunja serekali ambayo rais Mamadou Tandja aliunda kufuatia kura ya maoni iliyokua na utata mwezi Agosti mwaka jana.


Msemaji wa mapinduzi kanali Abdoul Karim Goukoye Karimou anasema, vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger viliamua kuchukua madaraka ili kukomesha hali ya mvutano wa kisiasa nchini humo.

Amesema hivi sasa Niger inaongozwa na baraza kuu la kudumisha demokrasia ambalo linatoa wito kwa wananchi kubaki watulivu na kuwa na umoja na kuifanya nchi yao kua mfano bora wa demokrasia, utawala bora na utulivu.

Rais Tandja alikua anakutana na baraza lake la mawaziri huko ikulu wakati mapinduzi yalipofanyika. Wanajeshi hivi sasa wanaripotiwa wanamshikilia katika kambi moja ya kijeshi nje ya mji mkuu.

Akizungumza na wandishi habari mjini addis ababa kamishana wa amani na usalama wa Umoja wa Afrika Ramtane Lamamra alisema umoja huo unafuatilia kwa karibu matokeo ya huko Niger.

Anasema daima wanakua na wasi wasi pakiwepo na ripoti ya matayarisho ya mapinduzi au kuwepo na kitishoi cha mapinduzi, kwani inakweda kinyumae na malengo ya umoja huo wa kupinga kuondolewa serekali kinyume cha katiba barani humo.

Rais Tandja amezidi kupoteza umashuhuri wake nchini NIger hasa baada ya kutumia kura ya maoni ya Agosti kubadilisha katiba na kuongeza muda wa mhula wake kwa miaka mitatu zaidi.

Viongozi wa mapinduzi wametangaza amri ya kutotoka nje usiku na wamefunga mipaka yote ya nchi kavu na anga ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG