Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:49

Dharuba yafunga kazi Mashariki ya Marekani


Sehemu kubwa ya kaskazini mashariki ya Marekani inakabiliana na hali mbaya kabisa ya hewa kutokana na dharuba kali ya theluji na upepo mkali, ikiwa dharuba ya pili kuu katika majira haya ya baridi yanayokumba pwani ya mashariki ya Marekani.

Wakazi kuanzia Washington, D.C. hadi mji mkuu wa biashara wa New York na maeneo ya kaskazini wameshauriwa kubaki majumbani kwa siku ya tatu mfululizo kutokana na dharuba kali ya tatu msimu huu.

Serekali kuu mjini Washington, imefungwa kwa siku ya tatu mfululizo na watumishi elfu 230 wamebaki nyumbani. Maelfu ya watu hawana umeme, tangu dharuba ya kwanza kutikisha eneo hilo wiki moja iliyopita kukiwepo karibu mita moja ya theluji iliyomwagika katika baadhi ya maeneo.

Shule zimefungwa katika eneo zima la masharikmi na hata jiji la New York ambalo ni nadra kufunga shule kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.

Bunge la Marekani halikukutana tangu Jumatano wiki iliyopita na kuahirisha kupigia kura miswada hadi baadae mwezi huu.

Idara ya kufuatilia hali ya hewa inaeleza kwamba Hali ya Washington, D.C. inakaribia kuweka rikodi ya kiwango cha juu cha theluji iliyomwagika katika mwaka mmoja tangu kuanza kuorodhesha matokeo ya hali ya hewa mara ya kwanza 1884.

XS
SM
MD
LG