Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:56

Makamu Rais Nigeria Apewa Madaraka


Bunge la Nigeria limempa madaraka Makamu Rais Goodluck Jonathan kuwa kiongozi wa nchi hiyo wakati Rais Umaru Yar'Adua anaendelea kupata matibabu nchini Saudi Arabia. Mabaraza yote mawili ya bunge yalipitisha mswaada Jumanne unaosema Bw Jonathan "kuanzia sasa atasisimia shughuli zote za ofisi ya rais, amiri jeshi mkuu wa majeshi...kama kaimu rais."

Baraza la Seneti la bunge hilo la Nigeria lilipitisha mswaada wa pili unaosema Bw Jonathan ataacha kuwa kaimu rais mara tu Bw Yar'Adua atakapolijulisha bunge kuwa amerejea kutoka likizo ya matibabu.

Katiba ya Nigeria inasema makamu rais anaweza kuchukua madaraka pale tu rais atakapoandika barua kwa bunge akisema kuwa hawezi kufanya kazi zake kama rais. Bw Yar'Adua hajaandika barua kama hiyo. Hata hivyo, Rais wa baraza la Seneti David Mark alisema Jumanne kuwa mahojiano aliyofanya Rais Yar'Adua na shirika la utangazaji la Uingereza - BBC - mwezi uliopita yalikuwa ushahidi kuwa yuko katika "likizo ya matibabu."

XS
SM
MD
LG