Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:43

Jacob Zuma alipa fidia


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali kuwa amepata mtoto na mwanamke ambaye si kati ya wake zake watatu.

Rais huyo alitoa taarifa Jumatano akisema kuwa ana uhusiano na Sonono Khoza mama wa mtoto huyo aliyezaliwa Oktoba. Ni mtoto wa 20 aliyezaliwa na kiongozi huyo wa miaka 67.

Katika taarifa amekubali kulipa fidia kwa familia ya Khoza.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kuliripotiwa na gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times.

XS
SM
MD
LG