Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:44

Mke wa kigogo Afrika Kusini akamatwa


Mke wa waziri wa usalama wa Taifa nchini Afrika kusini amekamatwa kwa madai ya kusafirisha madawa ya kulevya. Sheryl Cwele, mke wa waziri Siyabonga Cwele, alikamatwa kazini kwake katika halmashauri ya Hibiscus Coast, Ijumaa.

Sheryl Cwele anashtakiwa pamoja na raia mmoja wa Nigeria, Frank Nabolis, ambaye alikamatwa Afrika kusini mwezi Disemba.Watu hao wawili wanashutumiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Cocaine, wakiwatumia wasichana kama wauzaji haramu wa madawa.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba Sheryl Cwele amesema hana hatia. Mume wake pia amekanusha kufahamu mashtaka yeyote dhidi ya mke wake.

Kitengo cha taifa cha kuendesha mashtaka nchini humo kinasema Sheryl atabakia chini ya ulinzi mpaka kesi itakaposikilizwa tena Ijumaa ijayo.

Madai dhidi ya Sheryl Cwele yaliibuka mwaka jana, baada ya kushirikiana na mwanamke mmoja wa Afrika kusini ambaye alishtakiwa Brazil kwa kujaribu kusafirisha kwa magendo kilo 9.2 za madawa ya Cocaine nje ya nchi. Mwanamke huyo Tessa Beetge anatumikia kifungo cha miaka 8 jela huko Brazil. Cwele alikanusha uhusiano wowote na kesi hiyo.

XS
SM
MD
LG