Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 08:15

Ndege ya Ethiopia yaanguka Beirut


Maafisa wa safari za ndege huko Lebanon wamesema kwamba ndege ya shirika la ndege la Ethiopia imeanguka kwenye bahari ya Mediterranean muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege ya kimataifa wa Rafik Hariri huko Beirut, Jumatatu alfajiri.

Maafisa wanasema kulikuwepo na abiria 83 na wafanyakazi 7 ndani ya ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliyopotea kutoka mitambo ya radar muda mfupi tu baada ya kuruka. Mashahidi kwenye eneo la pwani wanaripoti kuona moto mkubwa wakati ndege ilipokua inaanguka baharini.

Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia, kutokea Beirut wakati wa mvua na upepo mkali, uliokua ukiendelea Lebanon kwa siku ya tano mfululizo. Jeshi la Lebanon na kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa walianza mara moja kutafuta mahala ndege ilipoangukia ili kutafuta ikiwa kuna watu walonusurika.

Maafisa hawakua na habari za sababu za ajali hiyo iliyotokea kiasi ya kilomita 3.5 magharibi mwa mji wa Na'ameh, uliyoko kilomita 15 kusini mwa mji wa Beirut.

XS
SM
MD
LG