Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:32

Chama kipya cha kisiasa chaundwa Tanzania


Chama kipya cha kisiasa kimejitokeza huko Tanzania wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa Rais na wa Bunge baadae mwaka huu.

Chama hicho kimeanzishwa na baadhi ya wanachama wa sasa katika chama tawala cha CCM, ambao wanakhofu wataondolewa kwa njama katika utaratibu wa kupata wagombea ndani ya chama hicho kutokana na tofauti za mtazamo zinazojitokeza hivi sasa miongoni mwa wanachama wa CCM.

Kuna shutma kwamba ndani ya chama cha CCM, kuna makundi yanayopingana na kupanga mikakati ya kuharibiana katika utaratibu wa kupata wagombea ndani ya chama hicho kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwaka huu.

Kufuatia hali hiyo hatimaye chama kinachohusishwa kuondoka kwa baadhi ya vigogo wa chama cha CCM, kinachojulikana kama Chama Cha Jamii-CCJ, kimewasilisha maombi ya usajili wake kwa msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, John Tendwa.

Sauti ya Amerika ilizungumza na katibu mkuu wa muda wa chama cha CCJ, Renatus Muhabi, ambaye hata hivyo alikana kuhusishwa kwa chama hicho na baadhi ya vigogo ndani ya chama cha CCM, wenye khofu ya kuenguliwa. Anasema, “chama hichi tumekiunda kwa makusudi mazima kwamba kiwe chama cha jamii, kwa maana kila mtanzania atakae jisikia kua na imani na chama hichi, atakae pendekezewa na sera zake basi anakaribishwa.”

XS
SM
MD
LG