Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 00:12

Obama kutoa hotuba juu ya hali ya Taifa


Rais wa Marekani Barack Obama anatazamiwa kutoa hotuba yake ya kwanza juu ya hali ya taifa Januari 27. Msemaji wa White House Robert Gibbs anasema rais atalihutubia mabaraza yote mawili ya bunge la Marekani jumatano ijayo. Hotuba yake hiyo itaonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni za Marekani na hata moja kwa moja kwenye tovuti ya ikulu www.whitehouse.gov.

Baada ya kuwa madarakani kwa mwaka mzima, bwana Obama anatazamiwa kuelezea ajenda zake kuu za kisheria na kipaumbele kwa maswala ya kitaifa kwa bunge na taifa la Marekani.

Utawala wake ulianza kwa kurithi uchumi uliodorora, vita viwili, na mjadala mkubwa juu ya mageuzi ya mfumo wa afya na hivi sasa janga la tetemeko la ardhi katika nchi ya Haiti.

Rais Obama alitazamia kukamilisha swala la kutia saini sheria ya mfumo wa mageuzi ya afya kabla ya hotuba yake hiyo. Lakini wabunge bado wanajadilia vipengele vya mwisho ili kuondoa tofauti zao.

XS
SM
MD
LG