Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:48

UN yatoa wito wa msaada zaidi Haiti


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anasema Haiti inahitaji msaada ambao "haujapata kutokea" kutoka jumuiya ya kimataifa kutokana na uharibifu mkubwa uliokumba nchi hiyo katika tetemeko la ardhi la wiki iliyopita.

Bwana Ban anakwenda Haiti leo Jumapili kujionea mwenyewe juhudi za msaada katika kile alichoita "moja ya maafa makubwa kupata kutokea duniani katika miongo kadha." Anasema kipaumbele cha Umoja wa Mataifa ni kuratibu juhudi za misaada, kutoa msaada unaohitajika haraka, na kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo.

Maafisa wa Haiti wanasema maiti zipatazo elfu 40 zimezikwa katika makaburi ya pamoja na kubashiri kuwa idadi ya watu waliokufa inaweza kufikia hata laki mbili. Wafanyakazi wa misaada wa kimataifa wanajitahidi kusambaza maji yanayohitajika sana, chakula na madawa kwa waathirika, siku tano baada ya tetemeko la ardhi kupiga Jumanne iliyopita.

XS
SM
MD
LG