Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:03

Sheikh kutoka Jamaica arudishwa Kenya


Sheikh mmoja mzaliwa wa Jamaica ambaye wiki iliyopita alifukuzwa nchini Kenya na kusafirishwa hadi Gambia amerejeshwa tena nchini Kenya.

Awali msomi huyo wa dini ya kiislam alihukumiwa na mahakamam moja ya Uingereza kwa shughuli za kigaidi. Katika mahojiano kwa njia ya simu yaliyoandaliwa na mawakili wake jumapili, mtu huyo aliyejitambulisha kama Abdullah el-Faisal, alisema kwamba anashikiliwa katika mahakama moja ya Nairobi.

Serikali ya Kenya ilimfukuza Imam huyo Alhamis wiki ya jana hadi Lagos, Nigeria ambapo hatimaye alitakiwa kupelekwa hadi nchini Gambia. Lakini el-Faisal alinukuliwa akisema kuwa shirika la ndege nchini Nigeria lilikataa kumpeleka Gambia na kwa hiyo ikabidi arejeshwe nchini Kenya.

Waziri wa uhamiaji wa Kenya, Otieno Kajwang, alisema el-faisal alichagua kwenda Gambia, baada ya nchi kadhaa ikiwemo Marekani kumnyima visa ya kurudi nchi aliyozaliwa ya Jamaica.

XS
SM
MD
LG