Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:13

Obama atangaza hatua zaidi kupambana na ugaidi


Rais Barack Obama wa Marekani amesema katika hotuba kwa taifa Alhamisi jioni kuwa idara za serikali ya Marekani zilishindwa “kuunganisha” maelezo ya upelelezi yaliyokusanywa kabla ya jaribio la kulipua ndege ya Marekani siku ya Krismas.

Rais Obama alisema kuwa katika dunia inayobadilika wakati wote, msitari wa mbele wa ulinzi ni upelelezi ambao unashirikisha idara zote za usalama na hatua kuchukuliwa.

Lakini alisema katika tukio hilo la siku ya Krismas ambapo kijana wa Mnigeria alijaribu kulipua ndege iliyokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Detroit, idara za usalama zilishindwa kufuatilia kwa nguvu habari ambazo zingeweza kufichua njama hiyo. Rais Obama alisema pia kuwa hata hivyo mwisho wa yote yeye ndiye mwenye kuwajibika utaratibu unaposhindwa kufanya kazi.

XS
SM
MD
LG