Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:05

Bi Clinton anasema Yemen ni kitisho kwa usalama wa Dunia


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton alionya Jumatatu kwamba, patakuwepo na athari za kimataifa kutokana na vita huko Yemen. Pamoja na juhudi zinazoendelea za vikosi vya al-Qaida kutumia nchi hiyo kama ngome kwa ajili ya mashmabulio ya kigaidi nje ya kanda hiyo.

Alieleza wasi wasi huo wakati wa mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mkuu wa Qatar Hamad Bin Jassim Jaber Al-THani, anatembelea Washington.

Viongozi wa mataifa ya magharibi wameieleza Yemen kua taifa linaloshindwa kudhibiti utawala wake, wakitaja vita vyake na waasi wanaotaka kujitenga huko kusini mwa nchi, wapiganaji wa ki-Shia kwenye mpaka na Saudia, na kuongezeka kwa wapiganaji wa al-Qaida.

Marekani Ufransa na Uingereza zilifunga afisi zao za ubalozi huko Yemen wiki hii kutokana na vitisho vya Al-Qaida. Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Sana'a, umetoa ujumbe kuwataka raia wa Marekani huko Yemen kuchukuwa tahadhri na kuwa wangalifu.

Kufungwa kwa afisi hizo kunafuatia ahadi zilizotolewa na mataifa hayo mawili kuimarisha msaada wao wa kupambana na ugaidi kwa serekali ya Yemen. Kwenye ukurasa wa tovuti wa ubalozi wa Marekani, maafisa wanaeleza kwamba vitisho vimetoka katika kundi la Al-Qaida huko Peninsula ya Arabia, linalohusishwa na jaribio la kulipua ndege ya kimarekani siku ya Krismasi.

Kufungwa kwa balozi hizo kunatokea siku moja baada ya Jenerali wa Kimarekani David Petraeus kutembelea Sana'a kujadili masuala ya usalama na Rais Ali Abdullah Saleh. Jenerlai huyo mwenye ushawishi na mkuu wa majeshi ya Marekani huko Afghanistan na Irak, alitangaza hivi karibuni kwamba, Washington itaongeza kwa mara dufu msaada wake wa usalama kwa taifa hilo maskini.

Uingereza imetangaza pia mipango ya kuungana na Marekani katika kugharimia juhudi za kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi huko Yemen. Pamoja na mipango ya kuandaa mkutano wa kimataifa juu ya usalama wa Yemen baadae mwezi huu.

XS
SM
MD
LG