Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 13:26

Tanzania Yaomboleza kifo cha Kawawa


Tanzania imetangaza maombolezo ya siku saba kufuatia kifo cha mmoja wa waasisi wa chama tawala cha CCM,mzee Rashidi Mfaume Kawawa ambaye alikuwa miongoni mwa waliopigania uhuru wa nchi hiyo.Kawawa alikuwa mshirika wa karibu wa baba wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere na aliwahi kushika wadhifa wa waziri mkuu na makamu wa rais wa Tanzania katika utawala wa Mwalimu Nyerere. Pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa C.C.M kabla ya kustaafu.

Alizaliwa Songea mwaka 1926. Alipata elimu ya msingi huko Songea na baadae jijini Dar-es-salaam. Alijiunga na masomo ya sekondari huko Tabora mwaka 1951-1956. Kawawa alikataa nafasi ya kuendelea na masomo ya juu katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ili kuweka bidii zake katika harakati za kugombania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Kawawa alifariki dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam Alhamisi asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo. Akiwa na umri wa miaka 83, ameacha watoto kadhaa na wajukuu.

XS
SM
MD
LG