Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 18:19

Tanzania: CCM yakanusha madai ya Chadema


Chama tawala cha Tanzania CCM kinakanusha katu kwamba hakijaagizia magari 200 ya aina ya Land Cruiser kama inavyo daiwa na chama cha upinzani Chadema.

Katibu mkuu wa CCM Bw Yusuf Makamba, amesema "akutukanae hakuchaguli tusi, kwanza sisi hatukuagizia magari 200, magari tunayotegemea ni 150. Yamekwisha fika magari 74, na tunategemea wiki ijayo magari mengine 76."

Bw Makamba anasema jambo la kwanza ni uwongo si magari 200, na kwamba mpaka hivi sasa wameshalipa karibu Sh bilioni moja milioni 720 na elfu 65 na 31. Anasema fedha hizo wamelipa ushuri kwa Mamlaka ya Mapato TRA.

Akijibu madai hayo Katibu Mkuu wa chama cha upinzani Chadema, Dk. Willbrod Slaa, aliyetoa tuhuma hizo kwanza hapo jana wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilole wilayani Korogwe, anasema chama tawala kinajulikana kwa kukanusha tuhuma dhidi yake.

Anasema tuhuma alizokwisha wahi kutangaza zimekuja kuthibitishwa baadae kwa hivyo ni juu ya chama cha CCM kutoa ushahidi wa kuaminika, kufuatana na habari za kuaminika walizopokea kutoka vyombo vya serekali kwamba wameagizia magari 200, na wanakataa kulipa ushuru hadi wakati tulipokua tunatayarisha ripoti hii.

Hata hivyo msemaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA Bw Protas Mmanda, anasema kwa hakika hafahamu hizo habari zinatokea wapi lakini, kufuatana na uchunguzi wake ni kwamba "nilifuatilia kwenye rikodi zetu kuangalia ikiwa kweli ni magari 200 yaliyoingia mwezi huu wa kumi na mbili kama inavyo daiwa, lakini ukweli ni kwamba hakuna magari 200 yaliyoingia." Na ameongezea kusema kwamba ni magari 74 yaliyoingia mwezi wa kumi na moja na yote yamelipiwa ushuru.

XS
SM
MD
LG