Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:39

Marekani yaisaidia Kenya kukabiliana na ukimwi


Serikali ya Marekani imetoa msaada wa zaidi ya dola bilioni mbili na nusu kuisaidia serikali ya Kenya katika mpango wa kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi. Balozi wa Marekani nchini Kenya, Michael Ranenburger, anasema serikali ya Marekani imetoa msaada huo ili kuzuia maambukizo mapya ya ugonjwa huo wa ukimwi pamoja na maambukizo ya mama kwenda kwa mtoto.

Bwana Ranenburger, anasema msaada huu utatumika katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia hivi sasa. Hivi sasa asilimia saba ya wananchi wa Kenya tayari wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi. Anasema msaada huu utasaidia kuzuia maambukizo mapya hasa kwa watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu wa ukimwi, pamoja na watoto ambao hawajazaliwa.

Kwa miaka kadhaa iliyopita serikali ya Marekani na mataifa kadhaa ya magharibi, yamekuwa yakilalamika vikali kuhusu rushwa kwenye serikali ya Kenya na hasa matumizi mabaya ya misaada ya fedha inayotolewa na mataifa wafadhili.

Balozi huyo amesema hata hivyo hakuna kikwazo kitakachotolewa kwa Kenya kuhusu matumizi ya msaada huu wa fedha isipokuwa serikali ya nchi hiyo inatakiwa kuwajibika katika katika matumizi ya fedha hizo. Lakini anasisitiza kuwa serikali ya Marekani itasimamia matumizi ya fedha hizo.

XS
SM
MD
LG